NINJA APIGWA RUNGU LA MECHI 3 KISA KIWIKO, TFF YATOA TAMKO HILI KUHUSU RUFAA - TASMARA1

TAWI LA SIMBA SPORTS CLUB MKOANI MARA

TASMARA - TASMARA - TASMARA

AHSANTE SANA NA KARIBU TASMARA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

NINJA APIGWA RUNGU LA MECHI 3 KISA KIWIKO, TFF YATOA TAMKO HILI KUHUSU RUFAA

Share This
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Ofisa Habari wa TFF, imetangaza kumfungia mechi tatu mchezaji wa Yanga Abdalah Shaibu "Ninja'.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amesema Kamti hiyo imefikia maamuzi hayo baada ya kumchezea rafu kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union.

Ninja alimpiga kiwiki mchezaji wa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga Februari 2, 2019 na kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Licha ya adhabu hiyo kutolewa, Ninja aliitwa kwenye kamati kwa ajili ya mahojiano wiki kadhaa zilizopita na kukiri kuwa alitenda kosa hilo kisha kuomba msamaha.

Hata hivyo Kamati hiyo imesema Ninja na Yanga wanayo haki ya kukata rufaa kwani ipo wazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here