UONGOZI wa Real Madrid unataka kurudisha mmoja wa makocha wao wa zamani lakini wakitega karata yao kwa Zinedine Zidane au Jose Mourinho.
Hata hivyo, habari za ndani ya klabu hiyo zinasema kuna ugumu wa kumrudisha Zidane lakini Mourinho inadaiwa yupo tayari kukubali kibarua hicho, Real Madrid ipo bize inasaka kocha mpya kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo inayonolewa sasa na Santiago Solari.
Klabu hiyo inasemekana inataka kumwondoa Solari kabla ya kumalizika kwa msimu huu. Solari anaweza kuondolewa hata Real Madrid ikishinda mechi yao ya La Liga dhidi ya Real Valladolid, leo Jumapili.
Vigogo wa Real Madrid wanataka kocha wa kusuka upya kikosi hicho baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Copa del Rey na haina matumaini ya ubingwa wa La Liga msimu huu.
Zidane na Mourinho wote hawana kazi lakini wana masharti tofauti juu ya kazi hiyo. Mourinho alitimuliwa Manchester United mwezi Desemba mwaka jana wakati Zidane aliachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita.
Real imepata ugumu kwa Zidane kwani anataka fungu kubwa la usajili wakati Mourinho inadaiwa hana madai makubwa pengine suala gumu litakuwa mshahara wake.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
MADRID YATAKA MAKOCHA WAWILI
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Post Top Ad



No comments:
Post a Comment