
Timu ya Mwadui FC leo imekutana na kichapo kitakatifu kutoka kwa mabingwa wa soka nchini Simba SC wekundu wa msimbazi, mwadui fc wamekubwa na dhoruba hiyo katika mchezo mkali na wakuvutia ulio ungurumishwa katika uwanja wa taifa maarufu kwa mchina jijini Dar es salaam ambapo walisalimu amri ya mnyama Simba kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0.
mabao ya Simba yalitiwa nyavuni na Medie Kagere, Mzamiru Yasin na John Boko adebayo, magoli yote yalipachikwa nyavuni katika kipindi cha kwanza cha mchezo, hata hivyo vijana wa Mwadui walionyesha mchezo mzuri ingawa walizidiwa kwa kila idara.
Pengine mchezo huo ungemalizika kwa kushuhudia karamu ya magoli yasiyo pungua 5 kama safu ya ushambuliaji ya Simba wangekuwa makini katika umaliziaji.
Simba wanatakiwa kushinda takriban michezo yao yote zaidi 7 nyuma ya vinara wa ligi Yanga ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wanao ushikilia mpaka sasa. Timu ya yanga inaongoza ligi kwa alama 55.


No comments:
Post a Comment