Kikosi chetu jana jioni kiliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC katika mchezo mkali wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wetu wa Mo Simba Arena na kushuhudiwa na idadi kubwa ya mashabiki.
KMC ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 29 lililowekwa kimiani na mshambuliaji Charles Ilanfya baada ya kupokea pasi kutoka kwa Emmanuel Mvuyekure.
Bao hilo lilidumu kwa dakika sita pekee kwani nahodha John Bocco alitusawazishia baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Pascal Wawa.
Dakika ya 45 Bocco aliweka mpira kimiani baada ya kucheza gonga ndani ya 18 lakini hata hivyo mwamuzi Said Pambalelo alilikataa kwakua nahodha wetu tayari alikuwa kwenye nafasi ya kuotea.
Kiungo Jonas Mkude alishindwa kuendelea na mchezo huo dakika ya 53 baada ya kupata majeraha hali iliyopelekea kukimbizwa hospitali kwa msaada wa gari ya wagonjwa (Ambulance).
Nahodha Bocco alitupatia bao la pili dakika ya 74 baada ya shuti la kinda Cyprian Mpenye kupiga shuti lililo mgonga mlinda mlango Juma Kaseja kabla ya kukumkuta mfungaji.
Kiungo wa Simba, Said Ndemla (left), akichuana na kiungo wa KMC, Mohamed Samatta, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo jioni uwanja wa Mo Simba Arena. Simba ilishinda 3-1
Ibrahimu Ajibu alitupia bao kali la 'video' dakika ya 88 baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwa 'kuuchop' mpira na kumuacha mlinda mlango Jonathan Nahimana akiwa hana la kufanya.
Kikosi kilichoanza mechi dhidi ya KMC jioni ya leo ni tofauti kabisa na kile kilichoanza katika mchezo wa asubuhi dhidi ya Transit Camp na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.
Kikosi chetu kiliundwa na Aishi Manula, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Said Ndemla, John Bocco, Shiza Kichuya na Luis Miquissone.
Baadae Kocha Sven aliwaingiza Ajibu, Francis Kahata na Cyprian kuchukua nafasi za Mkude, Kichuya na Dilunga.
Beki wa Simba, Pascal Wawa, akimthibiti mchezaji wa KMC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo jioni uwanja wa Mo Simba Arena. Simba ilishinda 3-1 Winga wa Simba, Luis Miquissone, akichanja mbuga wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya KMC uliyochezwa leo jioni Uwanja wa Mo Simba Arena. Simba ilishinda 3-1 1
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment