Lugola awaonya Wanasiasa: Nitawashughulikia wote. - TASMARA1

TAWI LA SIMBA SPORTS CLUB MKOANI MARA

TASMARA - TASMARA - TASMARA

AHSANTE SANA NA KARIBU TASMARA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Lugola awaonya Wanasiasa: Nitawashughulikia wote.

Share This

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wanasiasa ambao wanafanya mikutano ya ndani ambayo imepigwa marufuku.
Ametoa kauli hiyo akiwa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na wananchi wa Mjini Kilosa ambapo amesema ana taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanaofanya vikao vyao vya ndani huku wakitoa kauli ambazo zinaashiria uchochezi.
“Mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sitakubaliana na kiongozi wa chama chochote kuvunja agizo tulilolitoa nchi nzima kwa kutoruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ya siasa, na pia kupitia mikutano ya ndani ambayo inafanyika, baadhi ya wanasiasa wahuni wanamtukana Rais ambaye ndiyo kiongozi Mkuu wa nchi, mimi sitakubaliana na hilo,” amesema Lugola.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here