Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen wameongoza maelfu ya waombolezaji wakiwemo wananchi, watumishi wa wizara ya ardhi, viongozi wa dini, vyama vya siasa na viongozi wengine wa kiserikali .
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Stephen kebwe yeye akawaomba wananchi kuwa watulivu wakati huu wa maombolezo na kuvitaka vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali na kutenda haki huku naibu waziri katibu mkuu wa wizara ya ardhi akasema serikali itagharamia mahitaji yote muhimu kuhakikisha miili hiyo inazikwa kwa heshima zote.
Watumishi hao wamepoteza maisha Februari 23 mwaka huu majira ya jioni baada ya gari yao kuacha njia na kutumbukia katika mto Kikwawila wakati wakielekea Ifakara kutokea kijiji cha Kiberege wilayani humo kugawa hati milki za kimila ambapo watu wanne akiwemo dereva walinusurika na kupata majeraha. Miili ya watu wawili kati ya tisa imesafirishwa kwa ndege kupelekwa visiwa vya mafia na ukerewe kwa maziko huku miili saba ikisafirishwa kwa magari kupelekwa mikoa ya Mbeya na Morogoro.

No comments:
Post a Comment