
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Manyara ,imewapandisha kizimbani watu wanne kwa kosa la kukwepa kodi.
Naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Isdory Kyando amesema kesi hiyo namba CC.3/2019 ilifunguliwa Februari 22 mwaka huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara.
Naibu mkuu huyo amewataja washtakiwa,kuwa ni Nashon Odhiambo Macokecha ambaye alikuwa Afisa Wanyama Pori Halmashauri ya wilaya ya Babati, Erasto Belela Kou Mwenyekiti wa Kijiji Vilima Vitatu, Francis Mwaso Mbele,aliyekuwa Kaimu Katibu wa Jumuhiya ya Hifadhi ya Wanyama Pori Burunge na Samson Sylvester Rumende ambaye ni Wakili wa kujitegemea.
Amesema Washtakiwa wote hao wanashtakiwa kwa kosa la kukwepa kodi K/F cha 15(b) cha Sheria ya Magari (Ushuru wa Usajili namba 124/2006).
Aidha amesema mshtakiwa wa nne Samson Sylvester Rumende Wakili wa kujitegemea anashitakiwa kwa kosa la Kughushi K/F 333, 335(d)(i) na 337 vyote vya Kanuni ya Adhabu.
Washtakiwa walikana makosa yote.
Mshtakiwa wa pili na wanne walidhaminiwa, Mshtakiwa wa kwanza na watatu hawakuweza kufika mahakamani hivyo Mahakama imetoa hati za wito wahudhurie April 4 mwaka huu ambapo shauri limepangwa kwa ajili ya kutajwa.
No comments:
Post a Comment