Rais Trump ashtakiwa, 'kuzuia matumizi mabaya ya nguvu za Rais' - TASMARA1

TAWI LA SIMBA SPORTS CLUB MKOANI MARA

TASMARA - TASMARA - TASMARA

AHSANTE SANA NA KARIBU TASMARA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Rais Trump ashtakiwa, 'kuzuia matumizi mabaya ya nguvu za Rais'

Share This






Muungano wa majimbo 16 nchini Marekani yakiongozwa na California yameushtaki utawala wa Rais Donald Trump kuhusu uamuzi wa kutangaza hali ya dharura ili kukusanya fedha za ujenzi wa ukuta wa mpakani na Mexico.

Kesi hiyo imewasilishwa katika mahakama ya wilaya ya kaskazini katika jimbo la California. Hayo yanajiri siku kadhaa baada ya Trump kuidhinisha hali ya dharura, inayompa nguvu kulivuka bunge na kujipatia fedha kwa ujenzi huo  ambao ni ahadi kubwa aliyotoa wakati wa kampeni yake.

Mkuu wa sheria katika jimbo hilo la California Xavier Becerra amesema wanampeleka Trump mahakamani "kuzuia matumizi mabaya ya nguvu za rais".

"Tunamshtaki Trump kumzuia dhidi ya kuiba pesa za mlipa ushuru, zilizotengwa kisheria na bunge kwa watu wa majimbo yetu. Kwa wengi wetu, ofisi ya rais sio eneo la vioja ," aliongeza

Kei hio iliyowasilishwa Jumatatu inaanza kwa kusikizwa awali ombi la kutaka kumzuia Trump ashughulikie dharura hiyo aliyoitangaza, wakati kesi ikiendelea kotini, gazeti la Washington Post linaripoti.







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here