Waandamanaji wakabiliana na polisi mjini London - TASMARA1

TAWI LA SIMBA SPORTS CLUB MKOANI MARA

TASMARA - TASMARA - TASMARA

AHSANTE SANA NA KARIBU TASMARA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Waandamanaji wakabiliana na polisi mjini London

Share This
Flares and smoke bombs have been thrown in Trafalgar SquareHaki miliki ya pichaREUTERS
Polisi walishambuliwa kwa chupa wakati wa makabiliano kati yao na mamia ya waandamanaji mjini London, ambao walipuuza agizo la kutoshiriki maandamano.
Makundi ya watu yalikusanyika katikati ya mji mkuu,wakidai kuwa wanalinda sanamu dhidiya wanaharakati wanaopinga ubaguzi wa rangi.
Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi pia yamefanyika katika miji tofauti nchini humu ikiwa ni pamoja na mii wa London.
Polisi wameweka masharti dhidi ya makundi kadhaa, kufuatia vurugu mbaya zilizoshuhudiwa wikendi iliyopita.
Makundi kadhaa kutoka sehemu tofauti nchini, pamoja na wanaharakati wa mrengo wa kulia, yalisema yamekuja mjini London kulinda alama ya historia ya Uingereza.
Protesters outside ParliamentHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMamia ya watu wengi wao wazungu walikusanyika katika ukumbi wa ukumbusho wa Cenotaph katika eneo la Whitehall amble linapakana na sanamu ya Winston Churchill iliyopo karibu bunge.
Mamia ya watu wengi wao wazungu walikusanyika katika ukumbi wa ukumbusho wa Cenotaph katika eneo la Whitehall amble linapakana na sanamu ya Winston Churchill iliyopo karibu bunge.
Makabiliano yameripotiwa kati ya polisi na waandamanaji ambao walikuwa wakisema kwa pamoja "England" huku wakiinua mikono yao kuelekea walipo maafisa wa polisi.
Baadhi yao walifanikiwa kuvunja uzio wa chuma unaozunguka Cenotaph katika eneo la Whitehall na kuanza kuwarushia polisi milingoti ya umeme na vifaa vingine walipokuwa wakijaribu kuwadhibiti.
Waadamanaji hao baadae walielekea Trafalgar Square, ambapo walianza kurusha fataki kuelekeakwa makundi ya yatu.
Polisi walikuwa na kibarua kigumu kuwazuia wasifike katika bustani ya Hyde Park ambako kulikuwa na mandamano ya amani ya watu wanaopinga ubaguzi wa rangi.
Wasimamizi wa vugu vugu la Black Lives Matter walikuwa wametoa kwa watu kutoshiri maandamano ya kupinga ubaguzi yaliyopangwa wikendi hii kwa kuhofia huenda yangegongana na makundi ya marengo wa kulia.
Police are confronted by protestors in Whitehall near Parliament SquareHaki miliki ya pichaPA MEDIA
Image captionPolisi wakikabiliana waandamanaji nje ya bunge
Police form a barrier in front of anti-racist protesters near Leicester SquareHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Akitumia kanda ya video inayoonesha makabiliano kati ya polisi na waandamanji hao kwenye Twitter, Waziri wa ndani Priti Patel alisema ni "ujambazi usiokubalika".
"Mtu yeyote atakaye chochea vurugu ama kuharibu mali atachukuliwa hatua kali za kisheria ," aliandika.
"Ukatili dhidi ya maafisa wetu wa polisi hautavumiliwa."
Protesters take the knee in support of the Black Lives Matter movement as they march near Marble Arch in Central LondonHaki miliki ya pichaAFP
Black Lives Matter protest in NewcastleHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaandamano huko Newcastle
Protesters from Black Lives Matter take part in a silent vigil on Brighton PierHaki miliki ya pichaPA MEDIA
Activists congregated at the cenotaph in George Square in GlasgowHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMijini Glasgow
Sanamu ya Churchill imekingwa kwa kuhofia isiharibiwe , baada ya waandamanaji kusema kuwa inaashiria ''ubaguzi wa rangi'' katika maandamano ya wikendi iliyopita.
Mamia ya watu pia walikusanyika katika miji ya Glasgow, Bristol na Belfast Kama sehemu ya mpango wa ''kulindaa'' historia.
Maandamano kadhaa ya kupinga ubaguzi wa rangi pia yameandaliwa katika maeneo tofauti Uingereza, ikiwemo Brighton, Newcastle,
Umeshawahi kujiuliza kama sanamu zinastahili kuwepo?


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here