Ufyatuaji wa risasi Atlanta: Kifo cha Rayshard Brooks kimetangazwa kuwa ni mauaji - TASMARA1

TAWI LA SIMBA SPORTS CLUB MKOANI MARA

TASMARA - TASMARA - TASMARA

AHSANTE SANA NA KARIBU TASMARA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Ufyatuaji wa risasi Atlanta: Kifo cha Rayshard Brooks kimetangazwa kuwa ni mauaji

Share This
Rayshard Brooks alipoteza maisha siku ya Ijumaa baada ya kupigwa risasiHaki miliki ya pichaEPA
Uchunguzi wa madaktari Atlanta, Georgia, umetangaza kwamba kifo cha Mmarekani mweusi ni mauaji baada ya kupigwa risasi katika makabiliano na polisi.
Rayshard Brooks alikufa wakati wanatoroka maafisa wawili wazungu katika mgahawa eneo la kuegesha gari la mgahawa mmoja Ijumaa.
Maandamano yalianza baada ya kifo chake, wiki kadhaa baada ya mwanaume mwengine mweusi George Floyd, kuuawa mikononi mwa polisi huko Minneapolis.
Mauaji ya Rayshard Brooks raia mwengine mweusi yametokea wakati maandamano yanaendelea Marekani, na kidole cha lawama kikaelekezwa kwa utumiaji wa nguvu kupita kiasi.
Rayshard Brooks, 27, alipigwa risasi Ijumaa jioni, mamlaka imesema.
Mayor Keisha Lance Bottoms amesema Erika Shields amejiuzulu Jumamosi.
Waandamanaji huko Atlanta waliandamana barabara wikendi hii wakitoa wito wa hatua kuchukuliwa kufuatia kifo cha Bwana Brooks'.
Mgahawa wa Wendy ambao mwanaume huyo ameuawa pia umechomwa moto.
Katika kipindi cha wiki tatu, watu kote Marekani wamekuwa wakiandamana kufuatia kifo cha George Flyod, mwanaume mweusi aliyekufa mikononi mwa polisi.
Waandamanaji walikusanyika katikati ya jiji la Atlanta siku ya Jumamosi baada ya kifo cha BrookHaki miliki ya pichaEPA
Kilichotokea usiku wa Ijumaa
Idara ya uchunguzi ya Georgia inachunguza kifo cha Bwana Brooks na inatafuta video za kamera za usalama ndani ya mgahawa wa Wendy's na pia picha za mashuhuda.
Katika video ya mashuda, Bwana Brooks alionekana akiwa kalala sakafuni nje ya mgahawa wa Wendy's, akipambana na polisi wawili.
Aliikamata silaha ya polisi na kufanikiwa kukimbia. Afisa mwingine aliweza kutumia silaha ya umeme kumnasa Brooks, kisha polisi hao wawili walitoweka kwenye video hiyo.
Milio ya risasi kisha ikasikika na bwana Brooks alionekana akiwa amelala chini.
Alipelekwa hospitali lakini baadae alipoteza maisha. Mmoja wa polisi alitibiwa majeraha aliyoyapata kwenye tukio hilo.
Ofisi ya mwanasheria wa kaunti ya Fulton inafanya uchunguzi wake kuhusu tukio hilo, imesema katika taarifa yake.
Kilichotokea Jumamosi
Aidha Jumamosi, Meya Keisha Lance Bottoms alitangaza kwamba mkuu wa polisi wa Atlanta, Erika Shields amejiuzulu baada ya mwanaume mweusi aliyekuwa amelala kwenye gari lake kupigwa risasi nje ya mgahawa mmoja.
Erika Shields amehudumu kama mkuu wa polisi tangu Desemba 2016 na kufanyakazi katika idara ya polisi ya Atlanta kwa zaidi ya miaka 20. Ataendelea kuwa katika idara hiyo lakini atatekeleza majukumu mengine, Meya Bottoms amesema.
''Kwasababu ya kutamani kwake Atlanta kuwa mfano wa mabadiliko yanavyotakiwa kuwa katika nchi hii, Shields ameamua kujiuzulu nafasi ya ukuu wa polisi ili mji huo usonge mbele katika kuujenga upya uaminifu wa polisi kwa jamii nzima,'' Meya alieleza kwenye taarifa yake.
Mmoja wa maafisa wa polisi waliohusika kwenye shambulio, Garrett Rolfe, amefukuzwa kazi na mwingine, Devin Brosan, amebadilishiwa majukumu. Wote wawili wamelitumikia jeshi la polisi kwa miaka sita, na miaka miwili kwa jeshi la polisi jijini Atlanta.
Raia wamepokea vipi kifo cha mtu mwengine mweusi?
Jumamosi, maandamano yalifanyika na kufunga barabara kuu. Waandamanaji walichoma moto mgahawa mmoja huku polisi wakirusha mabomu ya risasi.
Afisa wa polisi aliyehusiska na ufyatuaji huo alitambuliwa kama Garrett Rolfe, 27. Amekuwa katika kikosi cha polisi kwa miaka saba.
Huyu ni afisa wa 48 kuhusika katika tukio la ufyatuaji wa risasi mwaka huu ambako kunachunguzwa na idara ya uchunguzi katika eneo la Georgia, kulingana na shirika la habari la ABC News. Na katika visa hivyo, watu 15 wameaga dunia.
A man spray paints a message onto the wall of a restaurant destroyed after the Atlanta police shooting on 12 JuneHaki miliki ya pichaEPA
Mawakili wanaowakilisha familia ya Brooks imesema afisa wa polisi hakuwa na haki ya kutumia nguvu kupita kiasi, akisema silaha aliyokuwa amekwapua bwana Brooks haikuwa silaha hatarishi.
''Huwezi kumfyatulia mtu risasi isipokuwa kama amekuelekezea silaha,'' Mwandesha mashtaka Chris Stewart alisema.
Waandamanaji walikusanyika nje ya mgahawa wa Wendy's siku ya Ijumaa, kwa mujibu wa New York Times.
Maandamano yalianza tena katikati ya mji wa Atlanta siku ya Jumamosi. Picha za maandamano zikiwa zimeandikwa jina la Brookes na Black Lives Matter zilionekana zikiwa zimebebwa na waandamanaji.
Watu mjini Atlanta tayari wamekuwa kwenye maandamano baada ya kifo cha George Floyd. Aliyekufa tarehe 25 mwezi Mei baada ya polisi wa Minneapolis kumkaba kwa goti lake kwa zaidi ya dakika nane. Afisa huyo amefukuzwa kazi na kushtakiwa kwa mauaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here