TASAC yaridhishwa na ukarabati wa MV Butiama na MV Victoria - TASMARA1

TAWI LA SIMBA SPORTS CLUB MKOANI MARA

TASMARA - TASMARA - TASMARA

AHSANTE SANA NA KARIBU TASMARA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

TASAC yaridhishwa na ukarabati wa MV Butiama na MV Victoria

Share This


Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) limeeleza kuridhishwa na ukarabati wa meli za MV-Victoria na Mv-Butiama zilizokuwa zinafanyiwa matengenezo na Kampuni ya KTMI kutoka nchini Korea ya Kusini kwa ushirikiano na Kampuni ya Songoro Marine katika bandari ya Mwanza Kusini.

Akizungumuza jijini Mwanza baada ya ukaguzi wa meli hizo Mkurugenzi wa Bodi TASAC, Kapteni Musa Mandia alisema kwa mjibu wa ukaguzi na tathimini waliyofanya wameridhishwa na kazi iliyofanyika na wanakiri kuwa pesa iliyotengwa na serikali kwa ajili ya kazi hiyo imetumika vizuri.

“Kama bodi tumekuja maalumu kujionea miradi inayofanyika kanda ya ziwa na tumefarijika kwa yale tuliyoyaona na tumeanzia kule kwenye ujenzi wa meli mpya tumeona jinsi ambavyo kazi inaendelea, tumepita kwenye chelezo tumeona jinsi ilivyoundwa, lakini tumejionea pia ukarabati wa meli ambazo zimepewa jina la MV-Victoria hapa kazi tu Mv Butiama hapa kazi tu.

“Binafsi kwa niaba ya bodi ya TASAC nitumie nafasi hii kumupongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa juhudi ambazo amazichukua kufufua vyombo hivi kwani MV-Victoria imeundwa mwaka 1962 lakini sasa imefufuliwa kwa msaada wa Korea ya Kusini na kwa kweli baada ya kuikagua kuanzia chumba cha kuendeshea mpaka kwenye vyumba vya injini hii meli imerudi upya kabisa.

“Meli hii kulingana na matengenezo yaliyofanyika inao uwezo wa kuishi miaka 50 mingine iwapo itatunzwa vizuri kwa hiyo ni jambo zuri sana na kiukweli mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) na timu yake wamefanya kazi kubwa sana inayoendana na pesa iliyotengwa na serikali” alisema Mandia.

Alisema taarifa kutoka MSCL inaonyesha hadi sasa ukarabati wa meli hiyo umefikia asilimia 98 na asilimia mbili zilizobakia ni kwa ajili ya kufanyia majaribio ya safari vyombo hivyo ambapo vinatarajia kuanza kazi rasmi tarehe 1 juliy na kulingana na ukaguzi uliofanywa na TASAC  wanaamini vyombo hivyo vitafanya kazi nzuri na kukidhi haja ya usafiri wa majini kwa mikoa ya kanda ya ziwa.

Aliongeza kuwa kilichokuwa kinasubiriwa hadi sasa ni wahandisi kutoka nchini Korea nao kuja kufanya ukaguzi wao ili watoe tathimini na kukabidhi mradi ambapo kikwazo kikubwa kwa wao kufika kwa wakati ilikuwa ni changamoto za kufungwa kwa anga lao kutokana na janga la virusi vya corona.

Mkurugenzi Mkuu wa MSCL, Eric Hamisi alisema wahandisi waliokuwa wanasubiriwa kutoka nchini Korea ya Kusini hadi sasa wameshaanza  kuwasili na tayari wameshawasili watano huku wengine wanne wakiwa wanasubiriwa ambao wakiwasili watafanya safari ya majaribio na MV-Victoria mpaka bukoba ili kuangalia uwezo wa injini na ndani ya wiki mbili kuanzia sasa kazi hiyo inatarajiwa kuwa imekamilika .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here