TASMARA
Tunapenda kuwaomba radhi wapenzi watazamaji, wasomaji na wafuatiliaji wote wa mtandao wetu wa TASMARA ndani na nje ya mkoa wa Mara kwa kutokuwepo hewani muda wa takriban mwezi mmoja sasa, hali hii tunaamini imewaumiza na kuwaathiri wadau wetu ambao kila siku mlikuwa hewani kutuwinda ili mpate habari zetu kupitia mitandao yetu ya Blog, youtube, na hata katika Facebook ambako kote huko hamkuweza kutupata na hasa kwa habari mpya ambazo mmezoea kuzipata katika vyombo vyetu hivi kwa wakati na habari zikiwa bado za moto.
Hali hii ilitokana na matatizo ambayo yalijitokeza na yakawa nje ya uwezo wetu, nahivyo kusababisha tusiwe hewani na kwa hiyo kusababisha usumbufu mkubwa kwenu ninyi wadau wetu.
Hatahivyo tunapenda kuwatangazia wadau wetu wote kwamba sasa tumerudi na tuko hewani muda wote na kwamba sasa habari zetu zitakuwa hewani na kwa wakati kama ambavyo imekuwa jadi yetu hapo kabla.
Uongozi wa TASMARA unaomba Radhi kwa usumbufu wowote ulio tokea kufuatia hali hiyo ambayo hatukuitegemea, tuaahidi kuendelea kuziboresha huduma zetu na kuizuia hali kama hii isijirudie tena.
Mungu awabariki wote na tunawatakia Eid Mubarak waislamu wote.
Ahsanteni sana
Imetolewa na
Khalfan O. Missima
Katibu wa TASMARA.
No comments:
Post a Comment