MBOWE NA MATIKO WATOKA JELA KWA DHAMANA - TASMARA1

TAWI LA SIMBA SPORTS CLUB MKOANI MARA

TASMARA - TASMARA - TASMARA

AHSANTE SANA NA KARIBU TASMARA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MBOWE NA MATIKO WATOKA JELA KWA DHAMANA

Share This
Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko waliishinda rufaa ya DPP
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika Mahakama kuu Dar es Salaam.
Mahakama Tanzania imetoa uamuzi leo katika kesi ya rufaa waliowasilisha viongozi wa upinzani Freeman Mbowe na Esther Matiko kupinga uamuzi wa hakimu wa kuwafutia dhamana katika kesi inayohusiana na maandamano dhidi ya serikali.
Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama cha upinzani, Chadema, na Esther Matiko, kiongozi wa chama hicho tawi la wanawake, wamekuwa kizuizini kwa kukiuka mashrati ya dhamana walioomba.
Walishutumiwa kwa kutofika mbele ya mahakama mara mbili walipotakiwa kwenda kukabiliwa na mashtaka dhidi yao, na kuchochea kufutiliwa mbali ombi la dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Novemba 23, mwaka jana.
Mahakama ya Rufaa Tanzania, mapema mwezi huu ilitupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.

Uamuzi huo uliandaliwa na jopo la Majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti wao, Jaji Stella Mgasha, Mwanaisha Kwariko na Gerald Ndika baada ya kusikiliza hoja za upande wa mashitaka na upande wa utetezi zilizowasilishwa Februari 18, mwaka huu.
Mbowe

Sababu ya rufaa ya DPP

Sababu za DPP kukata rufaa hiyo ilitokana na Novemba 23, 2018 wajibu maombi (Mbowe na Matiko) kupinga uamuzi wa kufutiwa dhamana mahakama ya Kisutu na siku iliyofuata upande wa utetezi ukiongozwa na Kibatala walikata rufaa kupinga maamuzi hayo.
Novemba 27, mwaka jana, Jaji Rumanyika aliona kuwa rufaa hiyo imepelekwa chini ya hati ya dharura hivyo aliagiza mwenendo wa shauri upelekwe mahakamani hapo pamoja na wahusika wapande zote wafike.
Pia walidai mahakama imekosea kuwafutia dhamana kwa sababu Novemba 12, mwaka huu Mbowe na Matiko walifika mahakamani bila kukamatwa na kuwa chini ya ulinzi.
Hata hivyo, Novemba 28, upande wa mashitaka na wa utetezi walifika mahakamani hapo na mapingamizi ya pande zote yalisikilizwa ikiwemo sababu nne za Mbowe na Matiko za kupinga uamuzi huo kwamba mahakama haijawapa nafasi wadhamini ya kujieleza kwa mujibu wa sheria.
Alidai masharti ya dhamana waliyopewa washitakiwa ni kinyume na sheria.
Hata hivyo, upande wa mashitaka uliomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa hiyo kwa sababu tatu ikiwemo warufani kushindwa kukata rufaa kupinga dhamana iliyotolewa na mahakama ya Kisutu na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza rufaa kwani taarifa ya kusudio la kukata rufaa imekosekana.
Kainda alisema Jaji Sam Rumanyika wa Mahakama Kuu alitimiza matakwa ya kisheria na si vinginevyo kwa kuelekeza mwenendo wa kesi ulioandikwa kwa mkono pande zote zipewe na kwa pamoja walikubaliana zitumike.
Alisisitiza kuwa inaelekeza kwamba mwenendo wa kesi uambatanishwe na rufaa husika lakini kama sivyo, Jaji amepewa mamlaka ya kuelekeza vinginenvyo.

''Hatuwezi kupingana na Jaji kwa uamuzi aliochukua wa kujulisha pande zote tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo na baada ya kubaini kuwa pande zote hazikuwa na mwenendo wa kesi hiyo aliagiza mwenendo huo wapewe pande zote,'' alisema Kainda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here