
Ajax ikicheza soka la kiwango cha hali ya juu, imefanikiwa kuiondosha mabingwa wa ulaya mara 13, Real Madrid katika uwanja wake wa nyumbani Bernabeu na kufuzu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 22.
Ikilala 2-1 katika mchezo wa kwanza, kikosi cha Erick ten Hag kilipata magoli ya mapema ndani ya dakika 18 kupitia kwa mshambuliaji wake Hakim Ziyech na David Neres.
Kiungo wa timu hiyo Dusan Tadic, alitengeneza mabao mawili , na kufunga goli la tatu kwa timu yake ya Ajax.
Real Madrid iliyokuwa inasaka taji la nne mfululizo la michuano hiyo, ilizinduka kwa goli la Marco Asensio katika dakika 20 za mwisho.
Lakini kiungo wa Ajax Lasse Schone kupitia mpira wa adhabu dakika mbili baadae , aliwanyamazisha vijana wa Santiago Solari ambao walihitaji kufunga magoli matatu zaidi ili kusonga mbele.
Gareth Bale ambaye alizomewa na mashabiki katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Barcelona, aliingia dakika ya 29 kuchukua nafasi ya Lucas Vazquez aliyeumia .
Mkosi uliendelea kuwakumba Real Madrid ambapo nyota wake Nacho alipewa kadi nyekundi katika dakika za lala salama.
Kwa ushindi huo Ajax inakuwa timu ya kwanza kufungwa nyumbani katika mchezo wa kwanza na kufanikiwa kupindua matokeo kwenye michuano ya ulaya.
Mchezaji bora wa mechi- Dusan Tadic (Ajax)

- Real Madrid inakuwa bingwa mtetezi wa kwanza kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya klabu bingwa ya ulaya tangu Chelsea ifanye hivyo msimu wa 2012-13.
No comments:
Post a Comment